Viwanja vya Maonesho ya Nane nane Nzuguni Dodoma |
Mkuu wa wilaya ya Chemba Saimon Odunga akiongea na wanahabari kutoka Dodoma na Singida. |
SERIKALI mkoani Dodoma imesema haitasita kuwachukulia hatua
viongozi wa Chama cha Wakulima (TASO) ambao wamekuwa wakipita kwa ajili ya
kuwatapeli wananchi licha na chama hicho kufutwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon
Odunga wakati akizungumza na waandishgi wa habari kwa niaba wakuu wa mikoa ya
Dodoma na Singida juu ya maonesho ya wakulima na wafugaji nanenane yanayoanza
leo katika viwanja vya Nzuguni Mjini hapa.
Odunga alisema TASO imefutwa lakini jambo la kushangaza kuna
waliokuwa watumishi wa chama hicho bado wanapita na kutapeli wananchi.
“TASO imefutwa kwa na msajili wa vyama vya hiari na wanatakiwa
kukabidhi mali kwenye serikali ya mkoa lakini hawakufanya hivyo, lakini kuna
wanaopita kutapeli wananchi na kuchgukua fedha jamboi hilo tunalichunguza na
tutachukua hatua” alisema
Alisema licha ya viongozo wa iliyokuwa TASO kutakiwa kukabidhi
mali zote ifikapo Julai 28, mwaka huu lakini hawakufanya hivyo na
wameandikiwa barua lakini hawakujibu ila wanapoteza muda tu hizo mali lazima
wakabidhi” alisema
Pia alisema wataanza kufanyia uhakiki wa viwanja ambavyo
vimetolewa na TASO.
“Kuna watu walipewa viwanja ndani ya maonesho lakini badala ya
kuvitumia wamegeuza makazi kwa kujenga nyumba za kuishi jambo hili halikubaliki
kwani maonesho hayo yapo kwa ajili ya kunufaisha wakulima na wafugaji na si
vinginevyo” alisema
Aidha alisema maandalizi kwa ajili ya maonesho hayo yamekamilika
na yatafunguliwa Agosti 3 na spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Job Ndugai.
Pia alisema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wanatarajia
kutembelea maonesho hayo ambapo nchi za Kenya na Uganga zimeleta washiriki.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo
ambayo yatakuwa na sehemu kubwa ya elimu kwa ajili ya wakulima na wafugaji.
Pia alisema wananchi watapa elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora
za bei nafuu.
Aidha alisema maonesho ya mwaka huu yameweka mfumo mzuri wa
kudhibiti mapato na kiingilio katika maonesho hayo kitakuwa ni Sh. 1,000 kwa
watu wazima na Sh. 500 kwa watoto.
0 Comments