Mh Diwani wa Mtisi Bw Emmanuel Sima akifunga mkutano wa wana SAPAWA kwaniaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida . |
Halmashauri
ya wilaya ya Singida,imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuajiri maafisa ugani
ngazi ya vijiji,ili kusongeza karibu zaidi huduma ya ugani kwa wakulima wadogo
na hasa wanawake.
Wito
huo umetolewa na kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Bw.Emmanuel Sima,wakati
akifunga jukwaa la wanawake wakulima wadogo,wanachama wa asasi ya
Sauti ya pamoja ya wanawake Singida (SAPAWA).
Amesema
kuwa uzoefu unaonyesha wazi kwamba maafisa ugani waliopo ngazi ya
kata,wameshindwa kuwafikia wakulima wote wadogo na hasa wanawake.
Akifafanua,Sima
ambaye ni diwani wa kata ya Musisi,amesema kata karibu zote zina vijiji zaidi
ya vitatu na kijiji kimoja kinakadiriwa kuwa na zaidi ya wakulima wadogo zaidi
ya elfu moja.
Afisa
shirika la ActionAid Tanzania kanda ya kati,Bw.Joramu Wimmo,amesema dodoso za
utafiti huo,ulilenga ushiriki wa watoa huduma,wapokea huduma na
viongozi mwenyeviti wa vitongoji, diwani
na wengine,lengo ni kuona kama makundi hayo yanafanya kazi kwa pamoja.
wajumbe mbalimbali wakisikiliza na kuchangia hoja katika mkutano huo uliokutanisha viongozi mabali mabali wa ngazi ya Serikati za vijiji ,kata,madiwani , mabalozi watendaji n.k. |
0 Comments