TIMU ya Singida United inatarajiwa kufika mjini hapa ijumaa
jioni julai saba mwaka huu,kwa ajili ya kujitambulisha kwa mashabiki wake na
kupata baraka zao.
Timu hiyo iliyofuzu kucheza ligi kuu msimu ujao,asubuhi ya
jumamosi julai nane inatarajiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa VETA
mjini hapa, na jioni yake itacheza mechi ya wao kwa wao.
Katibu wa timu hiyo
Abdalahamani Sima,alisema mechi hiyo lengo lake ni timu kujitambulisha rasmi,
mashabiki wake waweze kutambua majembe yao.
“Tumeona ni busara kubwa timu ikitambulishe kwa mashabi wake na
wadau wake kwanza,kabla kuanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu
msimu ujao.Kwa hali hiyo,natumia fursa hii kuwataka wapenzi wa soka na wapenda
michezo,kujitokeza kwa wingi kuja kuwaona wachezaji wao”,alisema Sima.
Akisisitiza,katibu huyo alisema wapenzi wa soka wakijitokeza kwa
wingi,kitendo hicho kitachochea ari ya wachezaji kupeperusha vema bendera ya
mkoa wa Singida, kipindi chote cha ligi kuu msimu ujao.
Sima alisema baada ya jumamosi,timu itaondoka kuelekea jijini
Mwanza kwa ajili ya kuweka kambi.
“Kama mnavyofahamu kwa sasa uwanja wetu wa namfua upo kwenye
ukarabati mkubwa,hivyo tunalazimika kutafuta uwanja nje ya mkoa.Tunatarajia
utakamilika kabla ligi kuu haijaanza,ili Singida michezo yake yote,ifanyikie
hapa nyumbani uwanja wa namfua”,alisema.
Wakati huo huo,Shabiki maarufu wa timu hiyo na mfanyabiashara
soko kuu mjini hapa,Robert Nyambi,alisema kuwa ingependeza zaidi kama Singida
United,ingecheza mechi na timu yo yote ya hapa mjini Singida.
0 Comments