Meneja wa ACTIONAID Singida na Chamwino Dodoma Elias Mtinga akizungumza na akinamama hao. |
Mgeni rasimi Mh Elia Digha mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Singida akipokea maandamano ya kina mama.
|
Wanawake
wametakiwa Kuungana kwa pamoja katika kutetea haki zao mbalimbali ili kukuza
uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Yemsemwa na
Irene Ndonde wakati akizungumza kwenye hafla uzinduzi wa umoja wa akina mama wa
mkoa wa Singida(SAPAWA) uliofanyika jana katika kata ya Ilongero katika
Halmashauri ya Singida.
Awali wanawake
hao wakisoma Risala yao wameeleza kuwa ipo Mikataba mbalimbali ambayo Tanzania
imeridhia ikiwemo ya kijinsia na umilikishwaji wa mali.
Kwa upande wake
Meneja wa Action AID Mkoa wa Singida na wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma
Bw.Elia Mtinga amesema kuwa lengo la Action AID ni kuwaunganisha akina mama
katika masuala mbalimbali huku akielezea Kongamano la wanawake Barani Afrika
lililofanyika jijini Arusha.
0 Comments