Mh Lazaro Nyarandu |
MBUNGE wa jimbo la Singida
kaskazini,Lazaro Samwel Nyalandu,anatarajia kuweka rekodi mkoani hapa, kwa
kutoa zawadi nono kwenye ligi ya soka ngazi ya kijiji,ya zawadi ya shilingi
mamilioni ya fedha.
Amesema anatarajia agosti mwaka huu
kuanzisha ligi itakayojulikana kwa jina la Kombe la Nyalandu.Mshindi wa kwanza
atazawadiwa shilingi milioni tatu tasilimu,jezi na mpira moja.
“Mshindi wa pili atazawadiwa shilingi
milioni mbili taslimu,jezi na mpira.Pia mshindi wa pili,atazawadiwa shilingi
milioni moja,jezi na mpira’alisema mbunge Nyalandu mbele ya kiongozi wa mbio za
mwenge wa uhuru zilizomalizika hivi karibuni mkoani hapa.
Kiwango hicho cha zawadi, ni kikubwa
mno kutolewa kwenye ligi daraja la kijijini mkoani hapa,toka nchi ipate uhuru.
Mbunge Nyalandu alisema ligi hiyo
itakuwa ni ya mpira wa miguu itakayoshirikisha timu ya wanaume na na timu ya
wanawake.
“Wanawake watacheza ligi yao ya
mpira wa miguu,hali kadhalika kwa upande wa wanaume,na wao watacheza ya
kwao”,alisema.
Mbunge huyo,ametumia fursa hiyo
kuwataka vijana wa kike na wakiume,kujitokeza kwa wingi kushiriki ligi hiyo
inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwa upande wake kiongozi wa kitaifa wa
mbio za mwenge,Amour Hamad Amour,amezitaka halmashauri za wilaya,manispaa na
majiji,kuandaa ligi kwa ajili ya kuibua vipaji na kuviendeleza.
0 Comments