Mkuu wa wilaya ya Mkalama Eng Jackson Masaka akiongea na wananchi kabla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika mbele ya Zahanati ya Mkalama.
|
Mbunge wa Mkalama Allan Kiula akiongea na wanachi kabla ya kutoa vitanda hivyo. |
Mh Allan kiula pia alitoamashuka kwaajili ya Zahanati hiyo ya Wilaya. |
Kimama wakifurahia msaada huo kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo. |
Baadhi ya
wananchi wilayani Mkalama wameitaka Serikali kuboresha huduma ya afya kwa
watoto na kwa mama wajawazito.
Hayo yamekuja siku moja toka
Mbunge wa jimbo hilo Bw,Allan Kiula kukabidhi vitanda 25 vya kulala wagonjwa na
vine vya kujifungulia kwa mama wajawazito vitakavyogawanywa katika
vituo mbalimbali vya afya wilayani humo
Mmoja ya wananchi hao
aliyejitambulisha kwa majina ya Khadija Ntunda ameushukru uongozi wa awamu ya
tano unaoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa hapo mwanzo
wamekuwa wakilala chini walipokuwa wakienda hospitali ili kupata matibabu na
hata kujifungua.
Kwa upande wake katibu wa umoja
wa wanawake Tanzania UWT kutoka kata ya Mwangeza Hamu Jofrey Msengi amesema
mbali na vitanda hivyo lakini pia Serikali hainabudi kuboresha huduma za watoto
hususani katika maeneo ya vijijini.
Naye mkuu wa wilaya hiyo mhandisi
Jackson Masaka amesema katika kuboresha huduma kwa watoto wizara ya afya ina
mpango wa kugawa vyandarua kwa mama wajawazito na watoto ili kutokomeza malaria
0 Comments