Na Grace Gwamagobe Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi leo ampokea madawati
2579 kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya mikoa ya
Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
Akipokea madawati hayo yaliyosafirishwa katika magari 19 ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Dkt Nchimbi amelipongeza jeshi hilo kwa
uzalendo huo wa kuhakikisha mali za umma zinafika Singida kwa ajili ya kuanza
kusambazwa katika halmashauri husika zikiwa salama na katika hali nzuri.
Dkt Nchimbi amelipongeza Bunge kwa uzalendo wa kumuunga mkono
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika
kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka nchini ili kutimiza azma ya kufikia
uchumi wa kati na wa viwanda.
Amesema madawati hayo yataongeza motisha kwa wanafunzi kujisomea
kwakuwa mazingira yatawawezesha kuandika na kusoma kwa ufanisi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishirikiana na
wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Askari wa Magereza
kushusha madawati yalitolewa na Bunge. Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika
mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
Askari wa Magereza wakipanda moja ya magari ya JWTZ na
kusaidia kushusha sehemu ya madawati 2579 yaliyopokelewa na Mkuu wa Mkoa wa
Singida kwa niaba ya mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa halmashauri ya Wilaya
ya Meru Frank Paul Mwambachi akisaidiana na askari wengine kubeba madawati
waliyopatiwa na Bunge ambapo halmashauri yake imepewa madawati 400.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimpongeza kwa
furaha mmoja wa mwanajeshi aliyehusika kusafirisha Madawati 2579 yaliyotolewa
na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mikoa ya Manyara, Arusha na
Kilimanjaro. Madawati hayo yamefikishwa Singida kwa ajili ya urahisi wa
kuyasambaza katika mikoa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipokea kwa
furaha moja ya magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyokuwa
yamebeba Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na
Kilimanjaro. Madawati hayo yametolewa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
0 Comments