Singida imemsajili Danny Usengimana kwa mkataba wa miaka
miwili akitokea Polisi.
Usengimana ndiye mfungaji bora misimu miwili mfululizo, alikuwa
mfungaji bora msimu uliopita lakini akarudia tena msimu huu baada ya kutundika
nyavuni mabao 19.
Singida United iliyopanda daraja msimu huu imekuwa ikisidi
kujiimarisha katika kila idara huku ikisajili wachezaji wa kimataifa wakiwemo
wale kutoka Zimbabwe.
Kikosi cha Singida United kinaongozwa na Kocha Hans van der
Pluijm ambaye amebeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga.
0 Comments