HAFLA za kufuturisha futari zilizofanyika na zinazoendelea
kufanyika mwezi huu mtakatifu wa Ramadhani,zimeonyesha wazi kwamba upendo na
mshikamano walionao Watanzani,bado upo imara kwa kizazi cha sasa,na pia
utaendelea kuwepo kwa kizazi kijacho.
Hayo yamesemwa juzi jioni na kaimu mkuu wa wilaya ya
Singida,Wilson Shimo,wakati akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na
diwani (CCM) kata ya Mitunduruni mjini hapa,Velerian Kimambo.
Alisema mikusanyiko ya hafla za kufuturisha,imekuwa ikikusanya
watu wa madhehebu ya dini na pia watu wenye itikadi za
kisiasa mbalimbali,bila kubaguana.
“Mfano mzuri na hai,ni hafla hii ya futari ya jioni hii.Hafla
hii imeandaliwa na diwani Kimambo ambaye ni mkristo.Lakini sijaona wala kusikia
watu wanaulizana wewe wa dini gani au umetoka chama gani cha siasa.Ni amani na
utulivu tu, ndio umetawala hapa”,alisema Shimo.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo,,alisema zipo nchi zingine
mikusanyiko ya aina hii ya kukusanya pamoja watu wa madhehebu ya dini na wa
vyama vya siasa tofauti,haipo.Zenyewe zimetawaliwa na vurungu na
kubaguana,basi.
Akisisitiza, alisema upendo na mshikamano unaoendelezwa na
Watanzania kwa sasa,uendelee kuenziwa na kudumishwa zaidi kwa faida ya
maendeleo ya taifa.
Aidha,Shimo ambaye ni katibu tawala wilaya ya Singida,ametumia
fursa hiyo kuwapongeza waumini wa dini ya kiislamu,kwa kutekeleza kwa ufanisi
maelekezo ya mtume Mohammed kwenye mfungo unaokaribia kufika ukingoni.
Kaimu mkuu huyo wa wilaya,amewataka wamalize kwa amani na
utulivu mfungo wa mwezi mtakatifu wa Ramadhani,na siku kuu ya Eid Elftir,isiwe
na vurungu za aina yo yote.
Kwa upande wake diwani Kimambo,amewasihi wakazi wa kata ya
Mitunduruni kuendeleza mshikamano uliopo,ili waweze kuunganisha nguvu zao
pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kata hiyo kongwe.
Katika hatua nyingine,amewataka kujitokeza kwa wingi kushiriki
mbio za mwenge wa uhuru utakaozindua vyumba vya madarasa ya kisasa katika shule
ya msingi Mitunduruni juni 30 mwaka huu.
“Tumepewa heshima mwaka huu Mwenge wa uhuru utalala kwenye kata
yetu.Tujitokeze kukesha na mwenge hapo katika shule yetu ya msingi
Mitunduruni”,alisema Kimambo.
Katibu tawala wilaya ya Singida Wilson Shimbu alipokuwa mgeni rasimi katika fututari iliyo andaliwa na Mh Kimambo diwani wa kata ya Mghanga maenoe ya Mji wa zamani. |
0 Comments