Wilaya ya Ikungi ni maalufu sana kwa kilimo cha VIAZI LISHE. |
Risala ilisomwa na Ibrahim Mluwa |
Mkuuwa mkoa Dr Rehema Nchimbi |
Ligi ya kina mama kuanza kutimua vumbi katika wilaya zote mkoani Singida Dr Nchimbi akabidhi mipira kwa maafisa michezo kila wilaya kwa maandalizi.
|
Singida kuku ni mboga ya kawaida. |
Ibrahim Mluwa akipokea zawadi |
Zawadi kutoka TANESCO |
WANANCHI mkoani Singida,wamempongeza rais Magufuli kwa
hatua yake ya ‘kunyoosha’ watumishi wa umma ambao kwa sasa,wamerejesha nidhamu
na uadilifu kwa kiwango cha kuridhisha.
Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi dunaini (mei mosi)mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi,amesema
pongezi hizo amepewa na wananchi mbalimbali na kwa nyakati tofauti.
Alisema wananchi hao kwa ujumla wao,wamesema chini ya
serikali ya awamu ya tano,watumishi wa umma,wamebadilika sana na sasa wanatoa
huduma kwa ukarimu mkubwa,wepesi na uharaka zaidi.
“Huko nyuma watumishi wa umma wengi walikuwa wana
urasimu wa hali ya juu.Walikuwa wakitoa huduma huku macho na akili zao zikiwa
kwenye ‘wathasp’.Mbaya zaidi mwananchi akipeleka kero zake,wanamwona ni
msumbufu.Hivi sasa mambo ni tofauti,kero za wananchi zinatafutiwa majibu na
majawabu kwa wakati”,alisema Dk.Nchimbi.
Hata hivyo,mkuu huyo wa mkoa,amesisitiza kwamba
watumishi wa umma wasibweteke waongeze bidii zaidi katika kuwatumikia
wananchi,ili pamoja na mambo mengine,waendelee kuipenda na kuiamini
serikali yao.
Katika hatua nyingine,Dk.Nchimbi amewakumbusha waajiri
juu ya wajibu wao wa kuwatambua,kuwathamini,kuwaheshimu na kuwapenda waajiriwa
wao.
Alisema kwa njia hiyo,miradi,huduma au shughuli yo yote
ya mwajiri itatekelezwa/itafanyika kwa ufanisi mkubwa.
“Ninyi wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na
manispaa,jengeni tabia ya kuwatambua wafanyakazi wenu.Wapendeni na muwathamini
wafanyakazi wote walio chini yenu.Hawa wafanyakazi mnaowaongoza,sio maadui
wenu,shirikianeni katika kuwatumikia wananchi”,alisema na kuongeza;
“Ukiona mtumishi anafanya mambo yanayokidhaza na
sheria,kanuni na utaratibu,usimkaripie wala kumtega,mtafutie afisa ustawi wa
jamii.Kwa vyo vyote afisa ustawi wa jamii atamrejesha kwenye mstari stahiki na
mambo yatakwenda vizuri”.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa,amekemea tabia mbaya ya baadhi
ya wakuu wa idara/vitengo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wafanyakazi wa kike walio chini yao.
“Wakuu hawa wa idara/vitengo wanakiuka sheria,kanuni na
taratibu kwa kuanzisha shughuli ya kimapenzi humo humo kazini.Wakati mwingine
wanafanya mapenzi na wake za watu.Tabia hii haikubaliki na haivumiliki hata
kidogo.Viongozi au wakuu wa idara/vitengo wenye tabia ya aina hii,waiache mara
moja”,alisema Dk.Nchimbi.
Pia Dk.Nchimbi amemwagiza mwenyekiti wa TUKUTA mkoani
hapa,kumpatia orodha ya majina ya watumishi wa umma wenye tabia mbaya ya
kuwapinga ovyo wake zao.
“Wapo wanaume ambao ni watumishi wa umma,wakiudhiwa
nje….hasira zote wanazipeleka nyumbani kwa mke wake na kuanza kumwangushia
vipigo vikali.Tukipata orodha yao,tutakaa nao kwa lengo la kuwarekebisha
tabia.Kama mume na mke hawaelewani,mwanaume husika hawezi kufanya kazi zake kwa
ufanisi.”amefafanua.
Wakati huo huo,mkuu huyo wa mkoa,amewahimiza watumishi
wa umma,wasikubali kuyumbishwa na wanasiasa.Wakikubali kuyumbishwa,ajira zao
zitakuwa hatarini.
Mmoja wa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo,Sombi
Hangida,alikiri kwamba ni kweli watumishi wa umma wamebadilika mno,na sasa
wanatoa huduma bila kuomba rushwa na wamekuwa na lugha rafiki kwa
wananchi.
0 Comments