JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI SINGIDA LAKAGUA MABASI YA SHULE

RTO mkoa wa Singida mrakibu wa polisi,Peter Raphael Majira,akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi,kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani.
Baadhi ya mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kati ya 20 yaliyofanyika ukaguzi jana (17/5/2017) na askari usalama barabarani,kwa lengo la kujiridhisha ubora wake.


Askari wa usalama barabarani mkoani hapa,  E.8763.Sgt.Benes Lucas,akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana (17/5/2017).

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Singida,limeanzisha zoezi la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, mrakibu Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza leo litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya ya sheria za usalama barabani, wakati  wote yanapokuwa barabarani.

Amesema wanatoa elimu na kukumbusha madereva na wamiliki wa mabasi juu ya wajibu wao kuzingatia kwa umakini mkubwa, sheria za usalama barabarani.

Aidha amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi,na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Kwa upande wao madereva hao, wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuendesha ukaguzi huo na kuwakumbusha juu ya sheria za usalama barabarani.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments