Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishauri jambo wakati wa kikao kifupi katika
Hospitali ya St. Gasper Itigi.
|
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi
ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo
kitaifa yatafanyika katika Hospitali ya St. Gasper halmashauri ya Wilaya ya
Itigi tarehe 12 Mei, 2017.
Dkt. Nchimbi amesema hayo mara baada ya
kukagua eneo la maadhimisho hayo pamoja na kukutana katika kikao kifupi na
watendaji wa chama cha wauguzi Tanzania na watendaji wa hospitali ya St Gasper
ambapo maadhimiyo hayo yatafanyika.
Amesema ana imani na uhakika kwa maadhimisho
hayo yatafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na maandalizi mazurri
yaliyofanyika huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye atawakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy
Mwalimu.
Dkt. Nchimbi amewataka wauguzi kuitumia siku
yao kuonyesha jinsi fani ya uuguzi ilivyokuwa ni fani ya upendo, huruma na
kujitoa sadaka katika kuhudumia jamii hivyo wauguzi hao wajitokeze kwa
wingi.
Ameongeza kuwa wananchi wote wa mkoa wa Singida
na wale wa halmashauri ya Itigi wajitokeze kwa wingi ili waweze kushirki
maadhimisho hayo kwa kupata huduma bure na ushauri juu ya masuala ya afya zao.
Kwa upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa
Singida Bi Theresia Ntui amesema maadhimisho ya siku ya wauguzi yatatanguliwa
na shughuli ya maonyesho ya shughuli za wauguzi.
Amesema maonyesho yatafanyika katika viwanja
vya hospitali ya St. Gasper kuanzia tarehe 10 mpaka 11 Mei 2017 ambapo kutakuwa
na huduma za bure kwa wananchi ambazo zitahusisha upimaji wa sukari, shinikizo
la damu, Virusi vya Ukimwi na mafunzo kwa vitengo juu ya utengenezaji wa uji wa
lishe kwa watoto.
Ameongeza kuwa wananchi wote hasa wazazi wote
kuhudhuria mafunzo hayo ya bure ambapo wataelekezwa hatua kwa hatua namna ya
utengenezaji wa uji bora wa lishe kwa kutumia vyakula asilia ambapo uji huo
utawasaidia watoto pamoja na watu wazima kuwa na afya njema.
Bi Theresia Ntui amewasihi wauguzi wote
Mkoani Singida na Mikoa ya jirani kuhudhuria maadhimsiho hayo ambapo wauguzi
wote watarudia kiapo chao cha uuguzi pia kutakuwa na maandamano ambapo
watakuwa na fursa ya kuonyesha maoni yao.
0 Comments