UZINDUZI WA CHANJO MKOA WA SINGIDA

Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Salum Manyatta

Mkoa wa Singida una jumla ya viyuo 221 vianavyotoa huduma za afya kati ya vituo hivyo, vituo 197 vinatoa huduma za chanjo kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5. Hii ni ongezeko la vituo 5 kutoka vituo 192 vilivyokuwa vinatoa huduma hiyo mwaka jana. juhudi zinaendelea za kuongeza vituo ili kufikisha huduma hii karibu zaidi na wananchi.


kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa mkoa wa Singida RMO Dr SAIDI MANYATTA katika uzinduzi wa chanjo mkoani Singida wakati akitoa taarifa fupi ya mkoa iliyo fanyika katika Hospitali ya Sokoine manispaa ya Singia.

Pia Dr Manyatta ametoa taarifa ya malaria  ya mkoa wa Singida katika kipindi cha januari-Desemba 2016, jumla ya wagonjwa 65,453 sawa na asilimia 6.04 ya wagonjwa  waliofika kupatiwa matinbabu ya nje waligundulika kuwa na viini vya ugonjwa huo katiak mkoa wa Singida.

Mgeni rasimi Mkuu wa wilaya ya Singida Bw Elias Trimo 
"Kinamam na watoto wote hakikisheni mnalala kwenye chandalua ili kujikinga na Malaria" kauli hiyo imetolew ana mkuu wa wilaya wakati akizindua chanjo kimkoa .





Mkuu wa wilaya akitoa chanjo
Mkuuwa wilaya ya Singida Elias Tarimo akipima 

Meya wa naispaa ya Singida akipima malaria.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments