Katibu mkuu wa Baraza la Michezo Taifa BMT Mahamed Kiganja |
SERIKALI kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) inatarajiwa kuwakutanisha viongozi wa klabu ya Simba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kutafuta suluhu baina yao.
Taarifa ya BMT leo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Mohammed Kiganja, imesema kwamba, Serikali haifurahishwi na malumbano yanayoendelea baina ya Simba na BMT.
“Kwa vyovyote vile, amani ya nchi ipewe kipaumbel kwa kuhakikisha kila mmoja wetu anaheshimu na kufuata sharia na kanuni ziliopo,”amesem Kiganja.
Kiganja amesema watazikutanisha pande zote mbili ili kutafuta suluhu ya kudumu baada ya malalamiko ya Simba kutosikilizwa na TFF katika madai na malalamiko yake mengi kwa muda mrefu.
Tamko hili la BMT linafuatia viongozi wa Simba, wakiongozwa na Rais wake, Evans Aveva kukutana na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe leo mjini Dodoma.
Wakati huo huo: Simba SC imesitisha maandamano waliyopanga kuyafanya Jumanne ijayo, baada ya tamko la Serikali leo.
Ikumbukwe Simba ilimuandikia barua Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro kuomba kibali cha kuandamana Jumanne.
Pamoja
na hayo, Kiganja ameagiza kwamba TFF na Simba wazingatie sheria na kanuni
katika kudai haki na kutoa haki kwa wakati na amesema ni vyema njia ya
mazungumzo ikatumika badala ya kulumbana kwenye vyombo vya habari, jambo ambalo
linaweza kuwachanganya mashabiki na linaweza kuhatarisha amani.
0 Comments