Maraisi wa Marekani na Mexico |
Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na
kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa
kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena Nieto
kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini Washngton.
Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia
mtangulizi wake Vicente Fox.
Bwana Fox amesema ana uhakika Mexico italipiza kisasi kwa kutoza kodi
bidhaa zitokazo Marekani, iwapo mipango hiyo ya Rais Trump itatimizwa.
Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa
kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump. Katika ziara yake nchini
Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo
amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za
uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.
Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia.
0 Comments