Sally Yates |
Rais wa Marekani, Donald Trump amemfuta kazi Kaimu Mwanasheria
Mkuu wa Marekani, Sally Yates saa chache baada ya kiongozi huyo kuwaagiza
Mawakili kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo vya kuingia Marekani raia wa
nchi saba zenye waislamu wengi.
Sally Yates aliyeteuliwa na Rais Obama alisema kuwa alitoa agizo
hilo kwa Mawakili sababu haamini kama zuio la raia kuingia Marekani ni halali.
Rais Trump Ijumaa alitia saini amri inayozuia raia kutoka
Somali, Sudan, Libya, Yemen, Iran, Syria na Iraq kuingia nchini Marekani ambapo
zuio hilo ni la siku 90.
Maandamano yamezuka maneneo mbalimbali ya Marekani huku
wakipinga zuio hilo. Wanadiplomasia wamesema kuwa zuio hilo huenda
likasababisha hatari zaidi kwa usalama wa Marekani.
Aidha, baadhi wamehoji kwanini zuio limewekwa kwa nchi
hizo saba wakati kwa miaka ya hivi karibuni hakuna raia wake aliyehusika na
ugaidi nchini Marekani?
Rais Trump amevikosoa vyombo vya habari vinavyopotosha
kuwa zuio hilo ni kwa Waislamu pekee. Rais Trump amesisitiza kuwa zuio
hilo ni kwa raia wote wanaotoka katika nchi hizo hata kama si Waislamu.
Trump alisaini amri hiyo katika kile alichosema kuwa ni kuzuia
watu wenye misimamo mikali kuingia nchini Marekani ikiwa ni hatua za kuimarisha
ulinzi na usalama.
0 Comments