Felix Simbu katikati baada ya kupata medali ya dhaabu Mumbai Marathon . |
Hapo baada ya kumaliza mbia hizo za nyika pembeni yake ni wakenya Joshua Kipkorir na Eluid Barngetuny . |
Felix Simbu ameshinda Mumbai Marathoni na kufanikiwa kupata
zawadi ya medali ya dhahabu na fedha taslimu dola 67,000 (Sh milioni 149).
Katika mbio hizo ambazo ni moja ya zile maarufu duniani, Simbu
alitumia muda wa 2:09:32
hadi alipomaliza, leo.
Mkenya Joshua Kipkorir ndiye alishika nafasi ya pili akiwa
amemaliza kwa tofauti ya sekunde 18 na Simbu.
Mkenya mwingine, Eluid Barngetuny naye alimaliza katika
nafasi ya tatu hivyo kumfanya Simbu kuwa kiboko ya Wakenya ambao wanasifika kwa
mbio hizo ndefu.
Katika hatua za mwisho Chesari, Bonsa Dida na Simbu ndiyo
walichuana vikali. Hata hivyo zikiwa zimebaki kilomita tano, taratibu Bonsa
alionekana kuchoka na kuwaacha Simbu na Chesari wakiendelea kuchuana vikali.
Kama unakumbuka Simbu anayedhaminiwa na Multichoice Tanzania
baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kumuombea,
alionyesha uwezo mkubwa tokea mwanzo wa mbio hizo za Mumbai nchini India.
Simbu amewashinda Wakenya na Waethiopia na sasa anapata nafasi
ya kushiriki michuano ya ubingwa wa dunia pamoja na London Marathoni.
Simbu anapokuwa kazini |
0 Comments