Katibu wa chama mkoa Bi Merry maziku katikati akiongoza zoezi la pushapu baada ya ushindi huo. |
Bi Merry maziku akiongea na wanachama makao makuu ya chama Singida mjini. |
Diwani mteule akibebwa juujuu baada ya ushindi. |
Wananchi wametakiwa kuendelea kudumisha amani na
kutumia haki yao ya kupiga kura ili kuwaweka madarakani watu watakao waletea Maendeleo
Katibu wa Chama Chamapinduzi CCM mkoa wa Singida
Bi, Merry Maziku amesema hayo wakati akizungumza kuhusiana na uchaguzi mdogo wa
udiwani uliofanyika katika Kata ya Kinampundu wilaya ya Mkalama
Bi, Maziku amewataka wananchi kuhakikisha
wanatumia shahada zao vizuri bila kushawishiwa na mtu ilikuweza kupata viongozi
bora.
Akizungumzia uchaguzi huo wa kata ya Kinampundu
amesema mgombea wa CCM bw,Slvester Marno ameshinda kwa kura 1409
Kwaupande wake diwani huyo Bw, Slvester Marno amehaidi
kushirikiana na wananchi wa kata hiyo ili kuharakisha maendeleo kutokana na
kasi ya serikali.
0 Comments