JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA LATAKIWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI


Jeshi la polisi mkoani Singida limetakiwa kutoa elimu na kuweka mikakati kwa watumiaji wa vyombo vya moto pamoja na watembea kwa miguu ili kupunguza ajali za barabarani.


Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe ameyasema hayo mapema leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.

Mtigumwe ameeleza kuwa viongozi wote  wa serikali waweze kuweka mikakati pamoja na kuzuia kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

Kwa upande mwingine amesema kuwa  kumekuwapo na baadhi ya polisi wanapenda kupokea rushwa  hivyo ameliagiza jeshi hilo kulitazama jambo hilo  kwa undani zaidi.
















Mayala Towo ni kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida amesema kuwa kutokana na maagizo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa watayatekeleza huku akiwataka watumia vyombo vya moto kitii sheria za barabarani.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments