Hadi anakutwa na umauti, Mashali alikuwa amepigana jumla ya mapambano 26
ya ngumi za kulipwa akishinda 19, kushindwa matano, sare moja na moja lilifutwa
ulingoni.
Enzi za uhai wake, Mashali alikuwa mkali kweli ulingoni akishinda mataji
tofauti kuanzia la Afrika Mashariki na KatiOktoba 14, mwaka 2012 kwa kumpiga
Med Sebyala wa Uganda kwa pointi ukumbi wa Friends Corner, Dar es Salaam.
Akalitetea taji hilo kwa kumpiga Mkenya Bernard Mackoliech Januari 12,
mwaka 2013, ukumbi wa Friends Corner, hivyo kupata nafasi ya kwenda kuwania
taji la IBF Afrika, ambalo hata hivyo alilikosa kwa kupigwa na Mtanzania
mwenzake, Francis Cheka Mei 1, mwaka 2013 kwa Knockout (KO) raundi ya saba
ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Mashali akashindwa pia kutwaa taji la Mabara la UB Novemba 16, mwaka
2013 baada ya kupigwa na Mrusi Arif Magomedov ukumbi wa Ivanhoe Country Club,
mjini Podolsk, Urusi kwa KO raundi ya saba.
Akasahihisha makosa yake na kufanikiwa kutwaa taji la UBO Afrika kwa
kumpiga kwa pointi Mtanzania mwenzake, Japhet Kaseba Machi 29, mwaka 2014
ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Akatetea taji hilo kwa kumpiga Alibaba Ramadhani Oktoba 5, mwaka 2014
kwa KO raundi ya tisa pambano la raundi 12 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kabla ya
kwenda kupigwa na Mrusi Apti Ustarkhanov kwa KO raundi ya pili ukumbi wa
Colosseum Sport Hall, mjini Grozny, Urusi Machi 5, 2016.
Mashali akarudisha heshima Mei 14 mwaka huu kwa kumpiga Sajjad Mehrabi
wa Iran kwa pointi Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam na kufanikiwa kutwaa
ubingwa wa dunia wa UBO uzito wa Super Middle.
Julai 9, mwaka huu alishindwa kutwaa taji la WBO Oriental uzito huo huo
wa Super Middle baada ya kupigwa na Mchina Zulpikar Maimaitiali kwa KO raundi
ya sita ukumbi wa Multi-Functional Hall, Water Cube mjini Beijing, China.
Akaweka kumbumbu ya
kushinda pambano la mwisho kabla ya kifo chake, kwa kumpiga Shaaban Kaoneka kwa
pointi ukumbi wa Chee Kwa Chee Pub, Bagamoyo mkowani Pwani Septemba 12, mwaka
huu.
0 Comments