Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amempigia simu rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma ,akimtaka kutupilia mbali uamuzi wa serikali kujiondoa katika
mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Afisi ya
bwana Ban imesema kuwa inathamini jukumu la taifa hilo katika kupigania haki na
kwamba inatumai taifa hilo litaangazia upya uamuzi wake.
Afrika
Kusini ilisema mapema mwezi huu kwamba itajiondoa katika mahakama ya ICC kwa
sababu ni kikwazo katika juhudi zake za kukuza amani barani Afrika.
Mwaka uliopita ,mahakama ya Afrika Kusini
iliikosoa serikali kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omar El bashir.
Mataifa ya
Burundi na Gambia tayari yametangaza kujiondoa katika mahakama hiyo.
Siku ya Ijumaa bwana Ban aliambia baraza la
usalama katika Umoja wa Mataifa kwamba alijutia mataifa yanayojiondoa katika mahakama
ya ICC kwa kuwa huenda yakatoa ujumbe m'baya kuhusu jukumu lao katika kupigania
haki.
0 Comments