Wananchi wanaotumia vyombo vya
usafiri wametakiwa kuwa makini na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka ya
usafirishaji wa majini na nchikavu SUMATRA ilikuweza kuepusha usumbufu wakati
wa safari.
Akiongea na standard redio
ofisini kwake meneja mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini
Sumatra Bw Michael polycap amesema katika kuelekea sikukuu ya krismasi na mwaka
mpya wapo baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wanao fanya udanganyifu.
Bw Michael polycap amewaomba
wasafiri kuhakikisha wanakata tiketi katika ofisi husika kwani zipo tiketi
bandia ambazo zinauzwa katika maeneo mbalimbali
Akizungumza kuhusiana na
wamiliki wa vyombo vya usafiri meneja huyo amewataka kuwa waaminifu na
kuhakikisha wanazingatia vigezo Sumatra pamoja na usalama barabarani.
Amesema katika kuadhimisha
sikuku hizi ni vyema wadau wakakumbuka kaulimbiu inayotumika kuanzia siku ya
maadhimisho ya uasalama barabarani ya Hatutakia ajari tunataka kuishi.
0 Comments