SHILINGI BILIONI MOJA ZAGHARAMIA UJENZI WA BARABARA KILOMETA 1.8 SINGIDA

Stend kuu ya mabasi Misuna Singida 

Halmashauri ya manispa ya Singida, imetumia zaidi ya shilling billioni moja kugharamia ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1.8 kwa kiwango cha lami, kituo cha mabasi madogo Majengo na kituo cha mabasi ya mikoani Misuna kati ya januari mwaka huu, hadi sasa.
 Kati ya fedha hizo shilingi 76,480,000, ni malipo ya msimamizi wa mradi huo umefadhiliwa na beki ya dunia
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida Deus Luziga, amesema utekelezaji wa kazi kwa sasa, ni asilimia 65 ya lengo na kazi inaendelea vizuri.

Busongo amesema kiasi hicho ambacho kimeshalipwa, ni malipo ya awali kati ya shilingi 6,168,949,244.67 ambazo zitalipwa baada ya kukamilika kazi,kwa mujibu wa mkataba.
 Kaimu mkurugenzi huyo, amesema ujenzi huo unaotekelezwa na mkandarasi Hari Singh and Sons ltd ya mkoa wa Kilimanjaro, unatarajiwa kumalizika January nne mwakani  (2017)
 Katika hatua nyingine, kaimu mkurugenzi huyo, amesema wanatarajia kutumia zaidi ya shilingi 454.6 milioni, kwa mwaka fedha 2016/2017 kwa ajili ya kugharamia matengenezo mbalimbali ya barabara zake.
 Alitaja baadhi ya mategenezo ya kawaida yatafanywa kwenye barabara ya  Mwankoko- Mtamaa, barabara ya Mandewa na  Mughanga.

Amesema wanatarajia kujenga mifereji ya maji ya mvua kwenye barabara ya Sabasaba, Minga, Utemini (SIDO), Sokoine na Mitunduruni.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments