Ramani ya Tanzania na mipaka yake |
Ramani mpya iliyotolewa na Tanzania ambayo inaonyesha kuwa inaamiliki
nusu ya Ziwa linalozozaniwa la Malawi au Nyasa, imezua mzozo mpya na Malawi
ambayo inasema kuwa ramani hiyo sahihi.
Ramani ya Tanzania
inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya
yake, lakini Malawi nayo inadai kuwa eneo hilo lote ni lake.
Malawi imeomba Umoja wa Mataifa, Mungano wa Afrika na mashirika
mengine ya kimataifa kuingilia kati.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Malawi,
Rejoice Shumba amesema kuwa Malawi imeandika barua kwa mashirika makuu duniani
ikiyataka kupuuzilia mbali ramani ya Tanzania.
0 Comments