Add caption |
Wagonjwa
wa kisukari Mkoani Singida leo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya macho na
daktari bingwa wa macho katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari duniani
ikiwa na kauli mbiu ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya macho.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida Dokta Ramadhani Kabala
amewaambia wagonjwa wa kisukari waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi wa macho kuwa
maadhimisho hayo mwaka huu yamelenga kuzuia wagonjwa wasiathirike zaidi na
magonjwa yatokanayo kisukari.
Dokta
Kabala amesema ugonjwa wa kisukari hushambulia zaidi macho, figo na moyo hivyo
serikali imeweka mkazo wa kuwafanyia uchunguzi ili kubaini tatizo ili wapatiwe
matibabu mapema au kuzuia yasitokee kabisa kwa kufuata kanuni na taratibu za
ugonjwa huo.
Ameongeza
kuwa ugonjwa wa kisukari unawakumbusha watu kuishi kwa kufuata kanuni bora za
afya kama kula mlo kamili, kula matunda badala ya juisi zilizotengenezwa
viwandani, kufanya mazoezi na kupunguza vilevi na sigara hivyo wagonjwa wa
kisukari hawana togauti na watu wengine isipokuwa wao hushauriwa kufuata kanuni
hizo kwa umakini mkubwa.
Dokta
Kabala amewakumbusha kutumia dawa kwa kufuata usahuri wa daktari wao pamoja na
kuhudhuria kliniki za kisukari kwakuwa kliniki hizo zinawasaidia katika
kushauriana namna bora ya kuishi kwa kufuata masharti wananyopewa pamoja
kuelimishanzaidi juu ya ugonjwa huo.
Naye
Daktari bongwa wa macho Mkoani Singida Dokta Ngh’ungu Kuzenza amesema utaratibu
huo unasaidia kuzuia au kupunguza madhara ya ugonjwa wa kisukari kwakuwa wengi
watatambuliwa kabla hawajafikia hatua ya kupofuka.
Dokta
Kuzenza ameongeza kuwa changamoto kubwa ni watu wengi kutopima ugonjwa wa
kisukari mapema mpaka wanapougua na hivyo kujikuta wameshaathirika macho ndipo
hutafuta huduma.
Kwa upande
wake mmoja kati ya wagonjwa wa kisukari 76 waliopata huduma ya kibingwa ya
macho Bi Asha Selemani Waziri Mkazi wa Iguguno ameema serikali imeweka
utaratibu mzuri wa kuwapima macho ili waweze kupata tiba mapema.
Bi Waziri ameiomba serikali kuendelea kuweka utaratibu wa
kuwapima wagonjwa wa kisukari magonjwa mbalimbali kama moyo na figo huku
akiwashauri wagonjwa wa kisukari kufuata ushauri wanaopewa na wataalamu
wa afya.
0 Comments