Kama
ilivyoripotiwa hapo awali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya
kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya
Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini
ya miaka 17, mwaka huu lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kutokana
na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza
apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri kwa ajili
ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging
Resonance).
TFF
iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za
usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za
vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo
ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri.
Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini
Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana
usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy
ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko
"vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF
inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .
Kadhalika
Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.
0 Comments