Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameishambulia jamii ya Wasomali wanaoishi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani ,akiwalaumu kwa kueneza maoni yenye itikadi kali nchini humo.
Alitumia mfano wa kisa cha shambulio la kisu
lililotekelezwa na mhamiaji raia wa Somalia mnamo mwezi Septemba katika mji wa
St.Cloud ,akisema kuwa wakaazi wa Minnesota wameteseka vya kutosha.
Bwana Trump ambaye alikuwa katika ziara ya
kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumanne amesema kuwa iwapo atakuwa rais
atahakikisha kuwa wakaazi wa maeneo wanashauriwa kabla ya wakimbizi kupelekwa
ili kuishi.
"Viongozi wetu wana ujinga kiasi gani?
Wana Ujinga kiasi gani kuruhusu mambo kama haya kutokea? Hapa Minnesota
mumekabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na ukaguzi mbovu wa wakimbizi,
huku idadi kubwa ya Wasomali wakiingia katika jimbo hili bila wakaazi
kufahamishwa,bila usaidizi wenu ama hata ruhusa.
Huku wengine wakijiunga na kundi la
wapiganaji wa Islamic State na kueneza maono yao ya itikadi kali katika kila
pembe ya nchi pamoja na dunia nzima kwa jumla.
Kwa kweli ni vigumu kuamini na kila mtu
anasoma kuhusu mikasa inayotokea Minnesota...Mumeona kisa cha shambulio la kisu
katika eneo la St Cloud.
Serikali ya Trump haitasajili wakimbizi bila
usaidizi wa jamii ya eno hili.Hilo ndilo wanaweza kuwafanyia kwa sababu
mumeteseka vya kutosha."
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika
Jumanne 8 Novemba, 2016.
0 Comments