Wanyabiashara wa kuku wa kienyeji
mkoani Singida,wamejipatia mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, baada ya
kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha mwaka jana hadi sasa.
Kaimu
katibu tawala msaidizi, uchumi na uzalishaji Beatus Choaji,amesema hayo wakati
akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili, kwenye kikao cha kamati ya
ushauri (RCC) mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo
la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida
Amesema
mapato hayo yamepatikana baada ya kuku 151,242 kusafirishwa na kuuzwa nje ya
mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.
Amesisitiza
kuimarisha ufugaji kuku wa asili, halmashauri zote hazinabudi kutekeleza
mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka
Mapema
mkuu wa mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kikao hicho,mhandisi Mathew Mtigumwe,akifungua
kikao hicho,aliagiza kuwa wananchi wahamasishwe, ili wasiendelee kuuza chakula
walichovuna msimu uliopita ili kiweze kuwafikisha kwanye msimu ujao wa mavuno
0 Comments