Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida M.Towo
|
JESHI LA POLISI TANZANIA
OFISI YA
KAMANDA WA POLISI “M” SINGIDA
03.11.2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
(PRESS
RELEASE)
KUTOROSHA BINTI CHINI YA UANGALIZI WA
WAZAZI
MTUH: JAHA S/O RAMADHAN
KUVUNJA NYUMBA MCHANA NA KUIBA
WATUH: HUSSEIN S/O SALEHE NA HASSAN S/O
SALEHE
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI
WATUH: HUSSEIN S/O SALEHE NA HASSAN S/O
SALEHE
Mnamo tarehe 26/10/2016 majira ya saa 22:30 HUSSEIN
S/O SALEHE, MWARABU, MIAKA 47, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Msufini ambaye ni Baba
mzazi wa LEILA D/O HUSSEIN, MIAKA 19, MWARABU, Mkulima na Mkaazi wa Msufini,
alifika kituo cha Polisi Singida akiwa ameongozana na HASSAN S/O SALEHE, MIAKA
47, MWARABU, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Msufini ambaye ni Pacha wake ambapo
walitoa taarifa kuwa binti yao huyo ametoroshwa na kijana aitwaye JAHA S/O
RAMADHAN, MZIGUA, MIAKA 23, Mkulima na Mkaazi wa Misuna.
Mara baada ya taarifa hiyo kupokelewa Kituo cha Polisi
upelelezi ulianza mara moja kwa kupata maelezo toka kwa Baba mzazi wa Mtoto
ambaye alidai kuwa binti yao kwa wakati huo amepelekwa maeneo ya Minga kwa Mama
mzazi wa mtuhumiwa, Polisi walikwenda eneo hilo kwa kuongozwa na walalamikaji
lakini hawakufanikiwa kumpata mtuhumiwa baada ya kuhoji watu waliokuwa eneo
hilo walieleza kuwa mtuhumiwa pamoja na binti wameacha pikipiki hapo na kuondoka
na hawakueleza walipoelekea. Pikipiki hiyo iliachwa nyumbani kwa Mama wa
mtuhumiwa aitwaye MWANJAA D/O ATHUMAN, MNYIRAMBA, MIAKA 35, Mkulima na Mkaazi
wa Minga. Polisi walimchukua Mama huyo kwa mahojiano zaidi pamoja na pikipiki
kama kielelezo.
Ilipofika tarehe 27/10/2016 saa 7:00 mchana binti na
kijana huyo walijisalimisha Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa Singida na kueleza
kuwa waliamua kwenda Kiomboi Iramba kukwepa hasira za baba wa binti huyo,
wakiwa wanaelekea kwenye Ofisi za Mkuu wa Upelelezi Mkoa Singida wakati
wanashuka kwenye Bodaboda maeneo ya Round about ndogo ya Bomani walikutana na
wazazi wa binti huyo ambao ni HUSSEIN na HASSAN ambao walianza kumshambulia
Binti yao kwa ngumi na mateke na binti huyo aliweza kuokolewa na Askari waliokuwa
maeneo hayo na kumsaidia kufika ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa Singida.
Baada ya Mkuu wa Upelelezi kuwasikiliza pande zote mbili, Mama wa Mtuhumiwa
aliachiwa na kijana wake alihojiwa kwa tuhuma za kumtorosha binti pia Binti
huyo LEILA alihojiwa kama Mlalalmikaji
kutokana na kulalamika kuwa Wazazi wake wamempiga na kumburuza chini na anahisi
maumivu sehemu ya Mguu wa kushoto na alidai kuwa yeye ni mjamzito hivyo
ilitolewa amri akapimwe. Katika mahojiano Binti huyo alieleza kuwa yeye
hajatoroshwa bali JAHA S/O RAMADHAN ni mpenzi wake wa muda mrefu na anania ya
kumuoa isipokuwa wazazi wake hawamtaki JAHA kwani ni mswahili na ni “CHOKORAA”
huku wakimlazimisha kuolewa na mtu asiyemtaka ambaye yupo D’salaam, pia yeye si
mwanafunzi kwani shule amemaliza tangu 2014. Baada ya kufunguliwa Jalada la
Shambulio SI/IR/4729/2016, Binti alipelekwa Hospitali na Askari na alilazwa kwa
uchunguzi zaidi na ilipofika tarehe 01/11/2016 asubuhi mimba ilitoka, chanzo
hasa cha kutoka Mimba hiyo bado hakijafahamika kwani hatujapata na tunasubiri
taarifa ya dakitari aliyemfanyia uchunguzi.
Tarehe 28/10/2016 saa 17:00 JAHA S/O RAMADHAN
alidhaminiwa, na alipofika nyumbani kwake aligundua kuwa chumba chake
kilivunjwa na katika kufuatilia aliambiwa kuwa mchana wa tarehe 27/10/2016
HUSSEIN S/O SALEHE na HASSAN S/O SALEHE wakiwa na gari mbili za familia yao
walivunja mlango kisha kupakia vitu vyote vilivyokuwa ndani kwa madai amevipata
kwa pesa ambayo amekuwa akihongwa na Binti yao. Thamani ya mali waliyochukua
bado haijafahamika. Mtuhumiwa huyo alirudi tena kituoni na kufungua kesi ya
kuvunja mchana na Kuiba SI/IR/4704/2016 yahusika.
Upelelezi wa mashauri hayo bado unaendelea na
watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana.
0 Comments