Wahitimu wa chuo cha
uhasibu (TIA) katika Kampasi ya Kigoma, Mwanza na Singida wametakiwa
kuwa Wadilifu ili kuhakikisha mafunzo waliyoyapata yanaweza kuinufaisha jamii.
Akiongea katika mahafali ya chuo cha Uhasibu Tanzania kampasi ya Kigoma,
Mwanza na Singida yaliyofanyika katika kampasi ya Singida, Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. ASHATU KIJAJI amewataka wahitimu hao
kutanguliza uadilifu wakati wa kufanya
kazi zao.
Dkt. KIJAJI amesema nchi inahitaji watu wadilifu katika Nyanja mbalimbali ili kuweza
kufikia hatima yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha kuhusiana na suala la ajira Dkt, ASHATU
amewataka wahitimu hao kuitumia vyema elimu walioipata kwa kujiajili huku
wakiendelea kusuburi ajira kutoa serikalini.
Awali akisoma taarifa
kwa mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa bodi ya Uhasibu Bw, COSTANTINE MASHOKA
ametaja idadi ya wahitimu wote kwa kampas ya Kigoma,Mwanza na Singida kuwa ni
1,800 ambapo wanawake ni 787 sawa na 52.2 % na wanaume ni 721 sawa na 47.8%.
Add caption |
0 Comments