Walishiriki kwenye dhifa hiyo siku moja baada ya kushambuliana vikali
kwenye mdahalo wa mwisho wa runinga.
Bi Clinton alicheka sana Bw Trump alipomtania kuhusu hotuba za kulipwa
na pia uchunguzi wa FBI kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi
kwa shughuli rasmi.
Lakini Bw Trump alizomewa alipofanya mzaha kwamba mpinzani huyo wake huwachukia
Wakatoliki.
Dhifa hiyo ya Wakfu wa Ukumbusho wa Alfred E Smith mjini New York
hufanyika kila baada ya miaka minne na kuwashirikisha wagombea urais.
Kuna desturi kwamba wagombea husimama na kutaniana, lakini mwana huu
imeandaliwa wakati kumekuwa na uhasama mkubwa sana kwenye kampeni.
0 Comments