Serikali imepiga marufuku watani wa jadi Yanga na Simba kuutumia
Uwanja wa Taifa na zimetakiwa kutafuta viwanja vya kutumia.
Tamko hilo limetolewa na Serikali hivi punde baada ya Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kulieleza hilo wakati
akizungumza na waandishi wa habari
“Uwanja huu sasa hautatumika na Yanga na Simba, hawawezi kufanya
uharibifu huu wa makusudi huku wakijua kwamba uwanja huu ndani yake kuna kodi
za walipa kodi.
“Mmeona walichofanya na sasa wanaweza kutafuta sehemu ya kwenda
kucheza, watafute uwanja wa kutumia, hadi hapo tutakapoamua vinginevyo,”
alisema Nape.
"Wanaotakiwa kuutumia ni ukiwa mzuri na si kama ulivyo
sasa, wako wengine wastaarabu wanaweza kuutumia."
Mashabiki wa Simba waling'oa viti na kuvirusha uwanjani baada ya
Amissi Tambwe wa Yanga kufunga bao na kabla ya kufunga alikuwa ameshika lakini
mwamuzi hakuchukua uamuzi wowote.
Lakini mashabiki wa Yanga nao wakajibu mapigo ya kurusha viti baada ya Simba kusawazisha bao katika dakika ya 87 kupitia Shiza Kichuya.
Lakini mashabiki wa Yanga nao wakajibu mapigo ya kurusha viti baada ya Simba kusawazisha bao katika dakika ya 87 kupitia Shiza Kichuya.
0 Comments