MWEZI
JULAI, FC Barcelona ilitangaza kuwa Neymar amekubali Dili mpya ya Miaka Mitano
na Jana Mabingwa hao wa Spain wamethibitisha kuwa ameshaini.
Jana
Klabu ya Barcelona iliposti kwenye Mtandao wa Twitter Picha ya Mbrazil huyo na
Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, wakipeana mikono kuthibitisha Dili
imekamilika.
Neymar,
akiongea na Barça TV, alisema anasikia furaha kubwa kwa kusaini Mkataba mpya
kwani anajisikia yuko Nyumbani.
Alisema:
“Kabla sijaja Barcelona nilijua ni Klabu kubwa na ina Wachezaji wazuri sana na
hilo lilinipa wasiwasi. Lakini nilipofika tu nikagundua ni Watu wema na hilo
lilinigusa moyoni na kunisaidia kujisikia Nyumbani!”
-
Neymar amefunga Mabao 91 katika Mechi 150 tangu 2013.
Mwezi
Julai Barca ilithibitisha kuwa kwenye Mkataba huu Mpya na Neymar, ikiwa Klabu
nyingine itataka kumnunua katika Mwaka wa Kwanza wa Mkataba huo basi itapaswa
kulipa Euro Milioni 200, Mwaka wa Pili wa Mkataba Dau ni Euro Milioni 222 na
kwa Miaka Mitatu iliyobaki kwenye Mkataba Dau litakuwa Euro Milioni 250.
Neymar
alijiunga na Barca kutoka Santos ya Brazil Mwaka 2013 kwa Mkataba wa Miaka
Mitano na kuweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Copa del Rey mara 2 na UEFA
CHAMPIONZ LIGI 1.
0 Comments