Shughuli kubwa ya uhakika ilifanywa na Victor Wanyama kuakikisha wanapata ushindi au sare |
Tottenham imekosa
nafasi ya kusogea juu katika orodha ya Premier League - angalau kwa saa kadhaa
- baada ya kuzuiwa kwa sare ya 0-0 kwa wenyeji Bournemouth.
Bournemouth nusra wachukuwe uongozi wa mapema
wakati Charlie Daniels aliposukuma tobwe lililookolewa na Hugo Lloris, Kipa
huyo wa Spurs alifanikiwa kuuzuia mpira na miguu yake.
Licha ya kuwa wageni Spurs walijiimarisha
katika nusu ya pili ya echi wenyeji walikaba mchezo, huku kipa Artur Boruc
akimzuia Dele Alli na Danny Rose, wakati Benik Afobe wa Bournemouth alipoingia
uwanjani karibu kipindi cha mwisho.
Wakati huo huo refa Craig Pawson aliwauadhi
mashambiki wa nyumbani waliohisi Lamela angepaswa kuonyeshwa kadi ya njano ya
pili, huku naye Moussa Sissoko hakuadhibiwa kwa kumdunga kisuku suku usoni
Harry Arter.
Pawson baadaye alikataa ombi la dakika ya
mwisho la Bournemouth kutaka penalti wakati Jack Wilshere alipoanguka baada ya
kuchengwa na Jan Vertonghen.
Makocha wote wamesifia umahiri wa timu
pinzani kuelekea kuanza mechi hiyo na haikushangaza mchezo ulivyoanza kwa kasi
kubwa na pande zote zikishambulia upande mpinzani kwa urahisi.
0 Comments