NAHODHA wa
Tanzania, Mbwana Ally Samatta ni kati ya wachezaji 30 walioingia kwenye orodha
ya awali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika.
Samatta
anayechezea KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, ameingia na wachezaji wawili wa
Afrika Mashariki kipa Mganda, Dennis Onyango anayechezea Mamelodi Sundowns ya
Afrika Kusini na kiungo Mkenya, Victor Wanyama anayechezea Tottenham Hotspur ya
England.
Orodha hiyo inaongozwa na Waalgeria watatu;
mshambuliaji wa mabingwa wa England, Riyad Mahrez, Islam Slimani wa Leicester
City na El Arabi Hillel Soudani wa Dinamo Zagreb.
Mkongwe
Samuel Eto’o anayechezea Antalyaspor ya Uturuki naye yumo kwenye orodha, pamoja
na Mcameroon mwenzake, Benjamin Mounkandjo wa Lorient.
Wengine ni
Serge Aurier (Ivory Coast na PSG), Eric Bailly (Ivory Coast na Manchester
City), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast na Hebei Fortune),
Mohamed Salah (Misri na Roma), Mohamed El Neny (Misri na Arsenal).
Wamo pia
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Dortmund), Andre Ayew (Ghana na West Ham),
William Jebor (Liberia na Wydad Athletic Club), Mehdi Benatia (Morocco na
Juventus), Hakim Ziyech (Morocco na Ajax), John Mikel Obi (Nigeria na Chelsea),
Kelechi Iheanacho (Nigeria na Manchester City).
Wengine ni
Ahmed Musa (Nigeria na Leicester City), Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal),
Yannick Bolasie (DRC na Everton), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Kalidou
Koulibaly (Senegal na Napoli), Keegan Dolly (Afrika Kusini na Mamelodi
Sundowns), Itumeleng Khune (Afrika Kusini na Kaizer Chiefs, Aymen
Abdennour wa Tunisia na Valencia, Wahbi Khazri (Tunisia na Sunderland) na
Khama Billiat (Zimbabwe na Mamelodi Sundowns).
Ikumbukwe
Samatta ndiye anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika aliyotwaa
Januari mwaka huu kufuatia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP
Mazembe ya DRC mwaka jana na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
Ni mafanikio
hayo yalimfanya anunuliwe na klabu ya Genk iliyoizidi kete Lyon ya Ufaransa na
klabu nyingine ziliokuwa zinataka huduma ya mchezaji huyo wa zamani wa Simba
SC.
0 Comments