WAFUNGWA MIAKA 30 KWA WIZI WA KUTUMIA SILAHA SINGIDA



Mahakama ya wilaya ya Singida imewahukumu watu sita kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyanganyi kwa kutumia silaha
Akisoma huku hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Joyce Minde amesema tukio hilo lilitokea January,24 mwaka 2016 majira ya saa tisa usiku katika kata ya mungumaji
Amewataja waliohukumiwa kuwa ni Yahaya  Mohamed(24),Yasin Shaban(29),Abdalah Shaban(28),Ablahaman Richard(26),Musa Hassan (25) na Gabriel Ibrahim(35).

Amesema watuhumiwa hao  walifanya kosa la unyanganyi na kujipatia shilingi million ishirini mali ya Ching Young  raia wa china ambapo ni kosa  na kinyume cha sheria kifungu cha 287 kifungu kidogo  A  cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Ameeleza kuwa hapo awali watuhumiwa walikuwa 9 lakini kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambapo washitakiwa watatu wameachiwa huru akiwemo Juma Athuman na Magadula Benjamin.

Kwa upande wa mwendesha mashita wa kesi hiyo Petrida Muta amesema kuwa mahakama iweze kuwapa adhabu ili kuwa fundisho kwa wengine wanaofanya kosa kama hilo
Kabla ya kutoa hukumu hiyo ametoa nafasi ya kujitetea kwa watuhumia ili kuweza kupunguziwa adhabu ambapo wamesema hawana cha kujitetea bali wanahitaji nakala za hukumu hiyo.


Hata hivyo baada ya kujitetea Hakimu Minde amesema mahakama inawatia Hatiani kwa kosa la unyanganyi kwa kutumia silaha

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments