MAN UNITED YAITWANGA FENERBAHCE!

Pogba na Lingard wakicheza kiduku baada ya kutupia
WAKIBADILI Wachezaji 7 toka Kikosi kilichoanza Mechi na Liverpool Jumatatu iliyopita, Manchester United Leo wameitandika Fenerbahce ya Uturuki Bao 4-1 Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya 3 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 31 kwa Penati ya Paul Pogba iliyotolewa baada ya Pasi ndefu ya Michael Carrick kumkuta Juan Mata ambae aliangushwa na Simon Kjaer.

Dakika 2 baadae Man United wakafunga Bao lao la Pili kwa Penati nyingine iliyopigwa na Anthony Martial baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Sener Ozbayrakli wakati akichanja mbuga kumuona Kipa alipoinasa Pasi ya Juan Mata.

Bao la 3 lilipigwa Dakika ya 45 kufuatia Rooney kuunasa Mpira na kumpasia Jesse Lingard aliemtengea Paul Pogba na kuachia kigongo cha Mita 20 hadi wavuni.
Hadi Mapumziko Man United 3 Fenerbahce 0.

MAN UNITED – Mechi zao za Kundi A:
MD 1 – Alhamisi Sep 15 – Feyenoord 0 Man United 1
MD 2 – Alhamisi Sep 29 22:05 –  Man United 1 Zorya Luhansk 0
MD 3 – Alhamisi Okt 20 22:05 – Man United 4 Fenerbahce SK 1
MD 4 – Alhamisi Nov 3 2000 –  Fenerbahce SK v Man United
MD 5 – Alhamisi Nov 24 2305 – Man United v Feyenoord
MD 6 – Alhamisi Des 8 2100 –  Zorya Luhansk v Man United

Dakika 3 baada ya Kipindi cha Pili kuanza, Man United waliandika Bao la 4 kwa Mpira ulioanza kwa Paul Pogba aliempasia Wayne Rooney ambae alimsogezea Jesse Lingard alieachia Shuti kali toka Mita 20 na kuingia wavuni.

Dakika ya 83, Robin van Persie, Mchezaji wa zamani wa Man United, aliipa Fenerbahce Bao lao pekee alipounganisha Krosi ya Emenike.

UEFA EUROPA LIGI
Matokeo:
Alhamisi Oktoba 20
KUNDI A
Feyenoord 1 Zorya Luhansk 0     
Man United 4 Fenerbahçe 1        
KUNDI B
BSC Young Boys 3 Apoel Nicosia 1        
Olympiakos 4 FC Astana 1
KUNDI C
FSV Mainz 1 Anderlecht 1 
Saint-Étienne 1 FK Qabala 0       
KUNDI D
AZ Alkmaar 1 Maccabi Tel-Aviv 2 
Dundalk 1 Zenit St Petersburg 2  
KUNDI E
AS Roma 3 Austria Vienna 3       
Viktoria Plzen 1 Astra Giurgiu 2   
KUNDI F
KRC Genk 2 Athletic Bilbao 0      
Rapid Vienna 1 Sassuolo 1
KUNDI G
Celta Vigo 2 Ajax 2 
Standard Liege 2 Panathinaikos 2
KUNDI H
Konyaspor 1 Sporting Braga 1     
Shakt Donetsk 5 KAA Gent 0
KUNDI I
FC RB Salzb 0 Nice 1        
FK Krasnodar 0 Schalke 1 
KUNDI J
FK Qarabag 2 PAOK Salonika 0   
Slovan Liberec 1 Fiorentina 3      
KUNDI K
Hapoel Be'er Sheva 0 Sparta Prague 1   
Inter Milan 1 Southampton 0       
KUNDI L
Osmanlispor 2 Villarreal 2 
Steaua Bucharest 1 FC Zürich 1   
TAREHE MUHIMU
Droo
26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16

17/03/17: Robo Fainali

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments