ZAIDI ya wajumbe 500 kutoka
nchi nzima pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya
nchi,kesho
wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Serikali za
Mitaa Tanzania(ALAT) utakaofanyika kwa siku 3 katika ukumbi wa mikutano wa
Kanisa Katoriki mjini Musoma ambapo hadi sasa asilimia kubwa ya wajumbe wa
mkutano huo uliodhaminiwa na benki ya NMB wameshafika mjini Musoma kwa mujibu
wa Makamu Mwenyekiti wa ALAT taifa,Stephene Mhapa
|
0 Comments