Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa
ni Makipa; Deogratius Munishi 'Dida' (Yanga SC), Said Kipao (JKT
Ruvu) na Aishi Manula (Azam FC).
Mabeki; Shomari Kapombe (Azam FC), Juma Abdul,
Andrew Vincent, Mwinyi Hajji (Yanga SC), Mohamed Hussein
'Tshabalala' (Simba SC), David Mwantika (Azam FC) na James Josephat
(Prisons).
Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mohammed 'Mo'
Ibrahim,
Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shiza
Kichuya (Simba SC), Simon Msuva, Juma Mahadhi (Yanga SC) na Hassan
Kabunda (Mwadui FC).
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco
(Azam FC), Mbwana Samatta KRC Genk (Ubelgiji), Elius Maguli (Oman)
na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Mchezo huo ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA), utafanyika mjini Addis Ababa, baada ya maombi
ya Shirikisho la Soka Ethiopia (EFF).
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana
kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora
na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya
nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi
ya 126.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana
Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk
inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani,
Colombia na Brazil.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora
duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
0 Comments