ASKARI WA AKIBA (MGAMBO)WACHEMWA KISU MNADANI

 


Ikungi

Na Mwadishi wetu

Askari wawili wa jeshi la akiba (mgambo) wakazi wa Kijiji cha Musimi kata ya Sepuka wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Ramadhani Salumu (23)na Hatibu Hemedi (25) wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kisu na nyuda Mdulu (23) mnadani baada ya mhalifu huyo kutakiwa kituo cha Polisi kutoa maelezo walipofanya vurugu mnadani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Musimi Omari Soa amesema Askari hao wa akiba wameshambuliwa na Nyuda Mdulu kwa kisu mnadani tarehe 30 Julai 2024 saa 10.00 jioni walipojaribu kutia chini ya ulinzi mtuhumiwa huyo  baada ya kufanya fujo mnadani Sepuka kwa wafanya biashara ndogondogo, wananchi na wafanya biashara katika eneo hilo waliweza kutoa ushirikiano kwa wanausalama hao nakufanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo.

Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo majeruhi walipelekwa kituo cha Afya Sepuka kutibiwa majeraha yao imefahamika |Ramadhani Salumu alichomwa kisu mkononi na mgongoni na kushonwa  nyuzi sita na Habibu Hemedi alichomwa kisu kwenye goti , ameshonwa nyuzi sita na wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri na mhalifu ameshikiliwa na Polisi Ikungi na baadae atafikishwa mahakamani.

Wananchi wa Kitongoji cha Musimi Magharibi anakoishi mtuhumiwa wamesema kijana huyo amekuwa na matukio mengi ya wizi na kugombana na watu hasa akiwa amelewa pombe na anafanya hivyo makossa ua uhalifu kwa faida yake.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Musimi Magharibi Juma Marughu amesema mwezi uliopita Nyuda Mdulu alifanya wizi  kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo hakukamatwa lakini nguo zilionekana zikifuliwa na mwenye nguo alizifahamu akapeleka taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho akaongozana na mwenye nguo hadi kituo cha Polisi Sepuka kutoa taarifa, walipofika nyumbani kwa Nyuda Mdulu katika upekuzi walikuta shuka moja wakaichukua kwa kielelezo, hata hivyo mhalifu hajakutwa alikutwa mama yake anayeitwa Hwa Rashidi nae akachukuliwa na  na Polisi hadi kituoni.

Katika maelezo yake kituoni sepuka Hawa Rashidi alikubali makossa ya kupatikana na nguo ya wizi nyumbani kwake zinazodaiwa kuibiwa na mwanae huyo akaandikisha maelezo yote na kukubaliana na mwenye nguo hizo alipe sh. 200,000/= na alishaanza kulipa kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Kitongoji Juma Marughu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Amon Kakwale amesema makosa ya  kisheria kushambuliwa askari wanaokuwa kazini, kosa jingine kuzuia askari wasifanye kazi wanazotumwa na Serikali na Zaidi mhalifu anajaribu kucheza na dola.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments