Dodoma
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima
Dendego amewataka Maafisa Ugani nchini kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa
Wakulima na Wafugaji kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wenye tija wenye kukidhi
masoko ya ndani ya kimataifa.
Wito huo ameutoa Agosti 5,2024 kwa niaba
ya Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko wakati wa ufunguzi wa mashindo ya Paredi
ya mifugo mbalimbali katika maonesho ya kimataifa ya Nane nane yanayofanyika
katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Aidha Mhe.Dendego amewasisitizia
vijana nchini kuchangamkia fursa ya programu ya BBT yenye lengo ya kuwanyayua vijana
kiuchumi kupitia kilimo
Nitoe rai kwa vijana wote nchini
kuchangamkia fursa hii ili kuongeza ajira na kukuza Uchumi wa mtu mmoja mmoja
na kwa taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao, Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Alexander Mnyeti na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde,
wamewahakikishia wananchi kuwa Serikali inaendelea kuweka mipango na mikakati
madhubuti ili kuhakikisha sekta hizo zinaongeza tija katika uzalishaji kama
hatua ya kuwaondoa wananchi na umaskini wa kipato.
Kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na
zaidi ya ng’ombe Milioni 37, Mbuzi Milioni 27.6, Kondoo Milioni 9.4 na Kuku
Milioni 103.
0 Comments