Mkuu wa Wilaya ya Singida Muhandisi Paskas Muragili akiongea katika kikao cha Baraza la madiwani.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili ametangaza oparesheni ya kukagua vyoo bora na watakaokutwa hawana vyoo bora watachukuliwa hatua za sheria.
Muragili ametangaza hatua hiyo kwa lengo la kudhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu unaosadikika kuwepo mkoani hapa.
Pamoja na kufanyika ukaguzi huo akaagiza kuundwa kamati za maafa zitakazosaidia kubaini na kuchukua tahadhari za kuepuka magonjwa hayo na maafa mengine.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elia Digha amesema katika oparesheni hiyo anatamani inanze na viongozi ikiwemo madiwani akidai kuwa baadhi ya Viongozi hao ambao ni kioo cha jamii hawana vyoo bora.
0 Comments