Waziri Juma Aweso akiwa katika Elikopta ya Mwekezaji wa Kilimo cha umwagiliaji cha Kijiji cha Choha Wilayani Ikungi Mkoani Singida ili kuoneshwa namna Teknolojia hiyo inavyo weza kufanya kazi.
Baada ya kupata melezo mafupi jkutoka kwa mwekezaji wa kampuni ya AL- PFRIDAWS kutoka nchini Jordan Ahmed Alkhatib Aljuu ya teknolijia ya uchimbaji wa Maji ili kuwezesha mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji kiweze kuanza uzalishaji.
Waziri Aweso akioneshwa matumizi ya Teknolojia hiyo kwa kutumia mtambo wa kisasa wa Radio Electromagic Frequency of thw water namna ya kutafuta maji chini ya miamba kwa umbali mlefu wa kuanzia mita 700 na kuendelea.
CHODA -IKUNGI
Wizara ya maji imeahidi kushirikiana na Kampuni ya AL FRIDAWS investment Company ambayo imekuja na teknolojia mpya ya kubaini maji yalipo na yanapatikana umbali upi chini ya ardhi.
Kampuni hiyo iliyowekeza mkoani hapa katika kijiji cha
Choda Wilaya ya Ikungi imekuja na ubunifu mpya wa utambuzi wa upatikana wa maji
ardhini kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji unaoitwa Pivot irrigation System.
Akizungumza
wakati alipotembelea Kampuni hiyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati wa
ziara yake amesema Teknolojia ambayo inatumiwa na Kampuni hiyo ni nzuri kwa
kuwa inatoa majibu ya uhakika katika Utambuzi wa maeneo yenye maji kabla
ya kuanza shughuli za uchimbaji.
Naye
Mkurugenzi wa rasilimali maji kutoka Wizara ya maji Dkt.George Rugomela amesema
teknolojia hiyo itakwenda kurahisisha upatikana wa maji kwa uhakika huku
akiomba teknolojia hiyo kufikishwa maeneo mbalimbali.
Aidha kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi ameeleza
kufurahishwa na teknolojia hiyo kwani itasaidia Wilaya hiyo kuondoa changamoto
ya upatikanaji wa maji kwa kiasi kikubwa.
Lengo la
ziara hiyo ya siku moja mkoani hapa imehusisha miradi 28 iliyopo mkoani katika
wilaya za Singida,Manyoni na Iramba katika mji wa Kiomboi sambamba na
kutembelea Mradi wa Kilimo wa kambupuni ya FRIDAWAS uliyopo wilaya ya Ikungi
katika kijiji cha Choda.
Baada ya kujionea teknolijia ya kisasa
inayoweza kufanya utafiti wa vitendo kwa njia ya anga kwa kutembelea maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na mji wa Kiomboi uliopo Wilaya ya Iramba Singida
ili kuona namna ya teknolojia hiyo inavyoweza kutumika katika maeneo mbalimbali
Nchini na kuleta ufumbuzi wa tatizo la upatikanaji wa maji.
Mkurugenzi
wa kampuni ya FRIDAWS Co.Ltd Ahmed
Alkhatib kutoka nchini Jordan ameipongeza ofisi ya Mkurugezi wa
Halmashauri na serikali kwa ujumla kwa ushirikiano anaupata mpaka sasa.
Kwa upande
wake katibu mkuu wizara ya Maji nchini Mwajuma Waziri amesema kuwa teknolojia iliyopo
imekuwa na changamoto hasa katika upatikanaji wa maji na kutokuwa na uwakika.
Awali
akimkaribisha mgeni rasimi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi afisa Tawala
wilaya hiyo Joseph Gathi amesema kuwa uwekezaji uliyowekezwa na FRIDAWS
unakwenda kufungua ajira kwa wakazi wa wilaya ya Ikungi.
0 Comments