Prof.Kitila Mkumbo Waziri wa Mipango akimwakilisha Dkt Mwigulu Nchemba kuwa Mgeni rasimi akiongea na kukabidhi michangongo yayao katika Harambee Hiyo ambapo Pref.Mkumbo alitoa zaidi ya milion 3 huku Dkt Mwigulu Nchemba akitoa Mil 5.
Mkuu wa Mko wa Singida Halima Dendego akitoa akiongea na wageni waalikwa na kukabidhi shili Mil 12 kwaniaba ya watumishi wa Serikali.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Dayosisi ya KKKT ya Kati Singida Mjini Dkt Cyprian Hilint akitoa neno la Jimbo la kati.
Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania Alex Malasusa akiongoza ibada Takatifu ya Harambee hiyo katika kanisa la Usharika wa Immanuel mjini Singida.
Mfanyabiashara Tesha Vunja beia akichangia katika harambee hiyo shili laki sita.Rais wa kijiji cha Nyuki Philemon Kiemi akichangia shilii laki tano.
Wabunge wa Mkoa wa Singida wakichangia zaidi ya Mil 12 kwa pamoja.
Burudani mbalimbali kutoka katika kwaya mbalimbali zikilindima.
Zaidi
ya sh. Milioni 800 ambapo fedha taslimu ni zaidi ya milioni 700 na ahadi ni
milioni 100 huku lengo lilikuwa ni kukusanya sh. Milioni 700 ili kuendeleza
vituo vya elimu vya Ihanja na Kiomboi, vituo vya afya, zahanati na hospitali
Singida mjini na Iambi pamoja na kuinua mfuko wa utumishi zikipatikana katika
misa takatifu ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kati usharika wa Singida Mjini.
Akiongea
katika harambe hiyo Profesa kitila Mkumbo waziri wa Mipango akimuakilisha Dkt
Mwigulu Nchemba aliyekuwa mgeni rasimi katiak harambee hiyo, alisema kuwa
hakuna namna nyingine ya kutokomezaumasikini isipokuwa kuwekeza katika elimu.
Prof.
Mkumbo amesema ili kujikomboa katika hali ya umaskini ni lazima jamii iwekeze
katika elimu maana elimu inasaidia hata katika kutafakari neno la Mungu na
kuliombea kanisa kuendelea kudumisha Amani, umoja na ushirikiano.
Aidha
ameeleza kuwa kanisa limetoa mchango mkubwa sana katika kuchangia maendeleo
nchini hasa katika sekta ya Elimu na Afya ambapo shule nyingi zimejengwa pamoja
na hospitali.
Awali
akimkaribisha mgeni ramsi mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amesema
serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini katika kuhakikisha
inawahudumia wananchi.
0 Comments