MPANGO WA SERIKALI NI KUHUDUMIA WATU WAKE -RC DENDEGO

 

Mkuu wa mkoa wa Singida Jalima Dendego Akiongea Katika izindizi wa Kituo cha Mafuta cha BUTL  kilichopo katika barabara kuu itokayo Dodoma Mwanza.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida.



Mkurugengi Mtendaji wa Kampuni ya BUTL Steven Mhele akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa na kwa Mkuu wa Mkoa waSingida.





Mpango wa Serikali ni kuhudumia watu wake na inaowajibu mkubwa wa kuweka sheria, sera na mipango na pia kushirikiana na sekta binafsi katika kutoa kuduma mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati akizindua kituo cha Mafuta cha kampuni ya BUTL kilichopo Mangua njuki kata ya Mandewa Manispaa ya Singida.

Dendego amesema kuwa kama viongozi wa Mkoa wilaya na maeneo yote kazi yao nikuweka mazingira mazuri ili sekta binafsi iweze kustawi na mwisho wa siku itaweza kutimiza ndoto ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe amesema kuwa ajenda na matamanio ya Mkuu wa Mkoa kuifanya Singida kuwa jiji hivyo basi ongezeko la uwekezaji katika Manispaa na Mkoa kwa ujumla utakuwa chachu ya kufikia vigezo.

Awali akisoma taarifa ya kampuni hiyo ya BUTL Meneja wa kituo hicho Milolous Chacha amesema kampuni hiyo katika ujenzi wa kituo hicho umechangia pato la mwananchi mmoja mmoja, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments