Mkuu wa Mjoa wa Singida Halima Dendego akiongea na Wakazi wa Mkoa wa Singida kupitia vyombo vya Habari.
Na Mwandishi Wetu
Mwenge wa Uhuru Unatarajia
kupokewa Mkoani Singida siku ya Tarehe 5/7/2024 katika Wilaya ya Manyoni
Ukitokea Mkoani Dodoma,Mapokezi hayo ya Mwenge wa Uhuru yatafanyika Chikuyu katika shule ya Msingi Wilayani
Manyoni mapema saa 12.00 asubui.
Akiongea na waandishi wa Habari Ofisini
kwake Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima
Dendego amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya zote 5 na
Halimashauri 7 kuanzia tarehe 5 na kukabidhiwa Mkoani manyara mnamo Tarehe 12.
Dendego amesema kuwa katika mkoa wa
Singida Mwenge wa Uhuru Utakimbizwa kwa Umbali wa Kilometa 800.75 na kutembelea
Miradi ya Maendelea 47, huku ujumbe wa Mwenge wa Mwaka huu ni “Kutunza Mazingira na Kushiriki Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa” sambamba na Jumbe za kudumu za Mwenge za
mapambano dhidi ya Rushwa na makongamano Mbalimbali.
Aidha Dedengo ameongeza kwa kusema kuwa
“Mwenge huu ni Mwenge Maalum wenye
kumbukumbu ya miaka 25 ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere na
Kumbukumbu ya Miaka 60 ya Mwenge wa Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano
wetu.”
Miradi ya Maendeleo itakayo Tembelewa na kuzinduliwa na kuwekwa
Mawe ya Msingi na Mwenge wa Uhuru katika
Wilaya zote 5 na Halmashauri 7 za Mkoa huu Itakuwa na dhamani ya Shilingi bili
100.12.
Akizungumzia Fedha mbalimbali zilizopatika Kwaajili ya Maandalizi
ya Mwenge wa Uhuru Kwa Mwaka huu Mkuu wa Mkoa Halima Dendego amesema kuwa
Wananchi wa Mkoa wa Singida wakichangia shilingi mili 287.442 huku Halmashauri
zikitoa shili Mili 677.837 fedha kutoka Serikali kuu Bili 30.582 fedha kutoka
kwa wahisani Bili 68.259 Wadau na Mbalimbali wa Mkoa wetu wa Singida wakitoa
Vifaa na fedha taslimu vyenye dhamani ya Shili 313.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Ametoa wito kwa wanachi kujitokeza kwa
wingi katika kuulaki mwenge huo utakapo fika katika maeneo yao katika Wilaya na
Halmashauri zote za Mkoa huu.
0 Comments