Watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha Hamis Ng'enyi mkazi wa GineryManispaa ya Singida wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Inaelezwa kuwa Siku chache zilizopita mtu mmoja mkazi wa Manispaa ya Singida aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa ndani ya nyumba yake na kupelekea kifo chake huku nyumba ikiteketea kwa moto.
Akisoma shitaka hilo hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Singida Allu Nzowa amesema kuwa washitakiwa Zurahina Hamisi mwenye umri wa miaka 21 pamoja na Hamidu Jumanne mwenye umri wa miaka 20 wote wakazi wa mtaa wa Manga Manispaa ya Singida wanakabiliwa na kosa la mauwaji ya kukusudia.
Amesema kuwa mnamo tarehe 2 juni, 2024 katika mtaa wa Unyankhae kata ya Mandewa Wilaya na Mkoa wa Singida watuhumiwa hao walimuua Hamisi Ng'enyi,hivyo wanakabiliwa na kosa hilo kwa mujibu wa kifungu namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Aidha kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 12 julay 2024 kwa ajili ya kusikilizwa na washitakiwa hao wako rumande.
0 Comments