Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Godfley Mnzava akiongea na wanachi Baada ya kumaliza mbio hizo katika Manispaa ya Singida.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amewataka wananchi kote nchini waasithubutu
kuchagua wagombea watakaotoa rushwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani
kufanya hivyo watachagua viongozi wabovu ambao hawataharakisha maendeleo kwenye
maeneo yao.
Kiongozi huyo wa mbio za
Mwenge ametoa kauli hiyo kwenye viwanja vya bombadia mjini Singida wakati
anazungumza mara mamia ya wananchi waliojitokeza baada ya risala ya Utii kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mnzava amewasisitiza
wananchi kuchagua Viongozi wenye sera na mipango madhubuti ya kuwaletea
maendeleo na sio viongozi wanatoa rushwa kwa sababu wakichaguliwa wataangalia
maslahi yao binafsi kuliko maendeleo ya wananchi.
"Msiwachague
Viongozi wanaotoa rushwa watawarudisha nyumba kwa sababu hatawaletea maendeleo
bali watajijali wao tu," Ameeeleza Mnzava.
Akizungumza na Vijana
zaidi ya 1000 kwenye Kongamano la Vijana mjini Singida, Kiongozi huyo wa mbio
za mwenge Uhuru Godfrey Mnzava amewahimiza Vijana kuwa wazalendo katika Taifa
lao na wadumishe amani na utulivu katika nchi yao.
Amewaomba vijana wenye
sifa na uwezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi
wa Serikali za Mitaa kwa sababu anaamini kuwa wanauwezo wa kufanya vizuri pindi
watakapochaguliwa.
Baadhi ya Vijana
walioshiriki kwenye Kongamano hilo wameiomba Serikali kuitisha mikutano na
makongamano kama hayo kwa sababu yatawasaidia kufahamu fursa mbalimbali za
kiuchumi zilizopo nchini pamoja kuwaimarisha kimaadili na kiuzalendo.
0 Comments