Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Godfley Mnzava akiongea baadaya kusomewa taarifa ya Ujenzi wa Bweni la wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali akitoa taarifa fupi kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili na kukimbizwa katika miradi mbalimbali wilayani Mkalama.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amekataa kuweka jiwe la msingi katika bweni la
wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani
Mkalama baada ya kubaini kuwa ujenzi wa bweni hilo na uzio unachunguzwa na
Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa -Takukuru- wilaya ya Mkalama.
Kiongozi huyo wa Mbio za
Mwenge wa uhuru amemwagiza Mkuu wa Takukuru wilaya ya Mkalama kumpatia taarifa
ya awali ya uchunguzi hapo kesho ili waweze kujiridhisha kuhusu uchunguzi
unaofanywa kwa sasa na Taasisi hiyo.
Ujenzi huo wa Bweni la
Wanafunzi wenye Mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani
Mkalama umegharimu zaidi ya shilingi milioni 140.
Mnzava pia amewataka
Watendaji wa Halmashauri ya Mkalama kumpatia taarifa kuhusu mchakato wa ukataji
wa bima za afya kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwenye shule ya msingi
darajani ili kujua kama kwenye kama gharama za kuwakatia bima wanafunzi hao
zimefuata taratibu.
Akiwa katika shule ya
Sekondari ya Mkalama One, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru ametoa muda
wa siku Saba kuanzia sasa kupatiwa taarifa kuhusu kwa nini ujenzi wa shule hiyo
ya Sekondari ya Mkalama haujakamilika licha ya Serikali kutoa zaidi ya shilingi
milioni 544.
Amesisitiza kuwa nia ya
Serikali ya kujenga shule za msingi na Sekondari nchini ni kusogeza huduma
karibu na wananchi hivyo ni muhimu kwa Watendaji kusimamia miradi hiyo
kikamilifu kulingana na thamani ya fedha na sio vinginevyo.
Awali akitoa taarifa
kuhusu miradi ya maendeleo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru, Mkuu wa
wilaya ya Mkalama Moses Machari amesema mwenge huo wa uhuru utatembelea,kukagua,
kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo Saba yenye Thamani
ya zaidi ya shilingi bilioni Mbili.
0 Comments