Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemaru Sanyamule akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego Mwenge wa Uhuru baada ya kukimbiza kwa siku nane Mkoani Dodoma ni katika Kijiji cha Cjhikuyu.
Sekta binafsi nichachu ya maendeleo hasa katika swala la
uwekezaji katika Nyanja mbalimbali Mkoa wa Singida tutahakikisha tunaendelea
kikaribisha wa wekezaji ili tuweze kufikia malengo tuliyo jiwekea.
Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imekuwa ikikaribisha na kutoa fursa kwa
wawekezaji wa ndani na nje ili
kutengeneza ajira na kuinua uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameyasema alipokuwa
akipokea mwenge wa uhuru Mkoa wa Singida kijiji cha Chikuyu Wilayani Manyoni.
Amesema kama Mkoa wanaendelea kuchachusha sekta binafsi katika
uwekezaji ambapo imechangia sh. Bilioni 67 katika miradi ya maendeleo itakayo
tembelewa, kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi na mwenge wa uhuru Mkoa wa
Singida.
Dendego ameeleza kuwa miradi yote 47 imegharimu zaidi ya sh.
Bilioni 100 ambayo inajumuisha sekta zote za elimu, afya, maji, mazingira,
elimu, kilimo na miundo mbinu.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati
akikabidhi mwenge huo Mkoa wa Singida amewapongeza viongozi wanaokimbiza mwenge
wa uhuru wakiongizwa na Godfrey Eliakimu kiongozi wa mbio hizo kitaifa kwa
kuelezea ujumbe wa mwenge, kuhamasisha shughuli za maendeleo ,kusisitiza
ufanisi na thamani ya fedha.
0 Comments